Serikali imetangaza amri ya kutotoka nje kwa siku 30 kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili alfajiri katika eneo la Chakama katika Kaunti ya Kilifi ambako Msitu wa Shakahola unapatikana huku uchunguzi ukiendelea.

Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki kupitia Notisi ya Gazeti rasmi la  serikali ametangaza eneo hilo kuwa eneo lenye misukosuko na eneo la uhalifu.

Amepiga marufuku mikusanyiko yoyote ya watu au maandamano kati ya 6 p.m. na saa 6 asubuhi kuanzia tarehe 26 Aprili.

Zaidi ya hayo, Kindiki amesema serikali imeanzisha Kituo cha taarifa, Ufuatiliaji na Msaada kwa Umma katika eneo hilo kwa ajili ya wale wanaotafuta wapendwa wao wanaoshukiwa kuwa sehemu ya dhehebu hiyo.

Yeyote aliye na maswali, taarifa au ripoti ya mtu aliyepotea ameshauriwa kupiga simu kwa nambari 0112 966 857.Idadi ya miili ambayo ilifukuliwa kufikia jana jioni ilikuwa 90.

April 26, 2023