BY ISAYA BURUGU,24TH NOV,2023-Siku moja baada ya matokeo ya mtihani wakitaifa wa darasa la nane mwaka huu KCPE kutangazwa ,watainiwa,wazazi na walimu wakuu wa shule mbali mbali nchini wanazidi kusherehekea ufanisi waliosajili katika mtihani huo.
Hali ni kam ahiyo katika kaunti hii ya Narok huku furaha,mbwembwe na vifijo vikitanda katika baadhi ya shule zilizofanya vyema.
Joy Lanoi ndie mwanafunzi bora kwenye mtihani huo katika shule ya msingi ya St Mary’s mjini Narok baada ya kujizolea alama 406 huku Morel Akinyi akizoa alama 400 kulingana na mwalimu wa shule hiyo mtawa Cosomo Mary amesema wanafunzi wa shule hiyo wameandikisha matokeo bora mwaka huu .
Katika shule nyingine inayomilikiwa na kanisa ST.Peters Catholic academy,pia sherehe zinazidi kuhushiwa baada ya mwanafunzi bora kupata alama ya wastani 410.Watainiwa watano kwenye shule hiyo walipata Zaidi ya alama 400 huku wale waliopata alama 399 hadi 350 wakiwa 48.Watainiwa 21 walipata kati ya alama 349 hadi 306.