Naibu Rais Rigathi Gachagua ametoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya washikadau wote wakiongozwa na sekta ya usalama na mahakama humu nchini ili kukomesha tishio la ugemaji, unywaji na vilevile uraibu wa pombe na dawa za kulevya katika eneo la mlima Kenya.

Naibu wa rais alieleza kwmaba hulka hii imehitilafiana kwa kiwango kikubwa na Maisha ya vijana katika ukanda huo na kuongeza kwamba taifa linakodolea macho na hatari ya kizazi kizima kuangamia iwapo hali hii haitadhibitiwa.

Gachagua aliyasema haya kutwa ya leo katika mkutano uliowaleta pamoja maafisa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, maafisa wa Utawala wa Kitaifa, Mamlaka ya ukusanyaji Ushuru nchini Pamoja na mamlaka ya kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya mongoni mwa mashirika mengine.

Zaidi ya hayo Naibu rais amebainisha kwamba serikali itahakikisha kwamba sheria mwafaka zinawekwa kabla ya mwezi Juni mwaka huu.

April 27, 2023