Shirika la Afya la duniani WHO linasema hivi karibuni litaanza majaribio ya chanjo moja au mbili dhidi ya aina ya virusi vya Ebola nchini Uganda.

Bodi ya afya inasema inasubiri idhini ya udhibiti kutoka kwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Ikiwa itaidhinishwa, chanjo hiyo inaweza kutekelezwa mwishoni mwa Oktoba au mapema mwezi ujao.

Huu ni mlipuko wa kwanza nchini Uganda kutoka kwa aina ya Sudan katika muongo mmoja.Wakati wa hatua ya kwanza ya utafiti, watafiti watakuwa wakijaribu usalama wa chanjo kwa kikundi kidogo cha watu.Chanjo zinazopatikana sasa zinafaa tu dhidi ya aina ya virusi vya Zaire, ambayo inahusika na milipuko katika nchi ya DR Congo na baadhi ya nchi za Afrika Magharibi.Wizara ya afya inasema sasa kuna kesi 43 zilizothibitishwa. Watu kumi wamefariki kutokana na ugonjwa huo miongoni mwao wahudumu wa afya wanne.

 

October 6, 2022