BY ISAYA BURUGU,1ST NOV,2022-Kama mojawapo ya njia za kupunguza makali ya ukame Caravan of hope linaloshirikisha wahisani wa kujitolea kwa hali na mali liligawa chakula cha thamani ya shilingi elfu mia tatu kwa familia 300 katikakijiji cha Lepolosi wadi ya Narosura- Majimoto,Narok kusini.
Wengi wa wakaazi walilazimika kutembea kwa masafa marefu ili kupokea chakula hicho.
Eunice Marima mkurugenzi mkuu wa Caravan of Hope na mwenye uzoefu wa maswala ya misaada alijuta kuwa takriban wakaaji 100,000 kaunti ya Narok wanaumia kutokana na makali ya ukame ikiwemo kufa kwa mifugo wao huku akiwarai wahisani zaidi kujitokeza na kutoa misaada kupitia makundi mbalimbali.
Naye kwa upande wake Julia Koikai mshirikishi mkuu wa Caravan of Hope aliwataka wanasiasa kutumia fursa hii kwa kuwashirikisha wajane na mashirika halali yaliyosajiliwa kugawa chakula.
Wiki iliyopita serikali kuu ilitoa magunia 3200 ya kilo 50 ya mchele na nyingine 1280 ya kilo 50 ya maharagwe kwa minajili ya kupunguza makali ya ukame kwa familia zilizoathirika.