Shirika la kutetea haki za binadamu nchini la Haki Africa limeelezea wasiwasi wake kuhusu kutumwa kwa maafisa wa usalama wa Kenya nchini Haiti kwa lengo la kulinda amani.
Kenya imetoa maafisa 1,000 wa polisi kuongoza kikosi cha usalama katika kupambana na magenge ambayo yametikisa mji mkuu wa nchi hiyo ya Caribbean Port-au-Prince kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Haki Africa imeibua maswali kuhusu usalama wa maafisa wa Kenya, ikitaja vizuizi vya lugha na uwezekano wa kulemewa na magenge hayo. Shirika hilo limeongeza kuwa ingawa kutumwa kwa maafisa hao tayari kumepitishwa,
serikali inastahili kuwa na miongozo ifaayo ya jinsi misheni hiyo itatekelezwa ili kuhakikisha maafisa wa Kenya wako salama.