Shirika la msalaba mwekundu nchini litafaidi na mgao wa shilingi milioni 100 kuanzia mwaka ujao wa kifedha kutoka kwa hazina ya kitaifa.
Hii ni mojawpao ya njia za serikali kuimarisha upatikanaji wa huduma za dharura kwa wakenya. Hatua hii inafuatia tangazo la rasis William Ruto, aliyeweka wazi kwamba serikali itarejesha mgao wa bajeti unaotengewa huduma na utendakazi wa shirika hilo.
Akizungumza katka ziara yake kwa shirika hilo eneo la South C mapema leo, Rais alieleza kwamba shirika hilo limekuwa na mchango mkubwa katika kuwasadia wakenya kujiinua hasa baada ya matatizo kama vile ukame, mafuriko na Mikasa mbalimbali.
GOVERNMENT REINSTATES BUDGETARY SUPPORT TO KENYA RED CROSS
The Government has reinstated its budgetary support to the Kenya Red Cross.
President @WilliamsRuto said the move has been informed by the huge humanitarian tasks that the Society engages in. – https://t.co/qWLteRbX3G pic.twitter.com/pTpT5xU2wA
— State House Kenya (@StateHouseKenya) April 20, 2023