Shughuli za kawaida katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JKIA zimesitishwa kwa muda kuanzia asubuhi ya leo, baada ya ndege ya mizigo iliyokuwa kwenye harakati za kupaa kupata hitilafu za kimitambo.
Mamlaka ya usimamizi wa viwanja vya ndege nchini KAA katika taarifa yake muda mfupi uliopita, imedhibitisha kusitishwa kwa shughuli zote za ndege kupaa au kutua katika uwanja huo huku juhudi zote zikiwekwa ili kurejesha hali ya usafiri wa kawaida.
Jambo! We would like to confirm that the runway at Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) has been temporarily closed due to an aborted takeoff by Cargo plane that developed technical issues this morning. 1/3
— Kenya Airports Authority (@KenyaAirports) April 17, 2023
Hadi wakati wa kuandaliwa kwa taarifa hii, shughuli za usafiri zilikua zimeanza kurejea japo kwa sehemu kidogo tu ya angatua hiyo.