BY ISAYA BURUGU,2ND OCT,2023-Shughuli za usafiri zimetatizika kwa muda mchana wa leo baada ya wananchi waliojawa ghadhabu kuandamana na kufunga bara bara kuu ya Narok-Mai Mahiu eneo la Duka moja kwenye kaunti ndogo ya Narok mashariki kulalamikia kile walichodai kuwa ongezeko la visa vya kihalifu sehemu hiyo.
Hii ni baada ya duka moja la Nguo kuvunjwa na nguo zenye dhamani ya shilingi elfu 70 kuibwa usiku wa kuamkia leo katika kituo cha kibiashara cha Duka Moja eneo hilo la Narok mashariki.
Ni hali iliyopelekea wananchi kuandamana na kufunga bada bara ya Narok-Mai Mahiu eneo hilo la Duka Moja hali iliyotatiza usafiri kwa muda sehemu hiyo wakilalamikia visa vya kihalifu sehemu hiyo na vile vile madai ya maafisa wa polisi kuchukuwa muda kufika walipoarifiwa kuhusu kisa hicho cha duka kuvunjwa.
Maafisa wa usalama baada ya muda mfupi walifika pale na kulazimika kutumia vitoa machozi kuwaondoa waandamanaji hao, na kwenye harakati hizo maafisa wawili wa polisi wakaaachwa na majeraha baada ya wananchi kuanza kuwalenga kwa mawe.
Hata hivyo, baadaye hali ilirejea kama kawaida baada ya viongozi wa usalama kwenye kaunti hiyo ya Narok mashariki wakiongozwa na kamanda wa polisi eneo hilo Jarred Marando kuingilia kati.