Shughuli za usafiri zingali kurejea katika hali ya kawaida kwenye barabara kuu ya Narok Kuelekea Mai Mahiu, baada ya barabara yenyewe kufungwa hio jana kutokana na ufa ulioshuhudiwa kilomita sita kutoka eneo la Mai Mahiu.
Kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka ya usimamizi wa barabara nchini KENHA, shughuli za ukarabati zitaendelea usiku kucha ili kuhakikisha kwamba barabara hiyo inarejelea hali ya kawaida na kuwapeusha wananchi pamoja na wachukuzi na hasara Zaidi.
Baadhi ya maafisa wa serikali akiwemo katibu wa maswala ya barabara Mhandisi Joseph Mbugua walizuru eneo hilo hii leo na kuahidi kuwa shughuli za usafiri ziaterejelewa adhuhuri ya kesho.
PUBLIC NOTICE
TRAFFIC UPDATE ON THE TEMPORARY CLOSURE OF MAI MAHIU – NAROK ROAD#kenhaalerts pic.twitter.com/g3svuVZFRX
— Kenya National Highways Authority (KeNHA) (@KeNHAKenya) May 1, 2023