Kila siku ya tarehe 16 mwezi Juni kuanzia mwaka wa 1991, ulimwengu huungana katika kuiadhimisha siku ya mtoto wa afrika. Katika maadhimisho ya siku hii, masuala mbalimbali yanayoathiri Maisha ya mamilioni ya Watoto katika bara la afrika hujadiliwa na uhamasisho kutolewa.
Mwaka wa 2024, suala la elimu lilipewa kipaumbele kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, kauli mbiu ikiwa ni Masomo kwa kila mtoto wa Afrika, wakati ni sasa. Kauli mbiu hii inaalika wahusika wa sekta mbalimbali kuimarisha juhudi za kuhakikisha kwamba kila mtoto anapata elimu.