Kinara wa Upinzani Raila Odinga amesisitiza kwa mara nyingine kwamba hana haja na salamu zozote za maridhiano au kupatana na serikali ya Kenya kwanza.
Odinga aliyezungumza kama mgeni katika kikao cha wajumbe wa chama cha Jubilee, amesema kwamba serikali ya kenya kwanza haina mantiki ya kukumbatiwa hivyo hakuna haja ya kutafuta mapatano yoyote.Katika hotuba yake, kiongozi huyo wa muungano wa Azimio la Umoja, amesema kwamba viongozi walio serikalini wanakosa usingizi kwa ajili ya mapatanano ambayo hana haja nayo.
Aidha amedokeza kwamba uovu wa utawala wa Kenya kwanza ulisababisha upinzani kutafuta majadiliano ya pande mbili, kama mojawapo ya njia za kutafuta haki itakayowasaidia wakenya. Hata hivyo, Odinga amesema iwapo mazungumzo hayo hayataonyesha dalili za kuafikia mapatano ya kuwasaida wakenya, basi mrengo huo utajiondoa.
Aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta awashutumu baadhi ya viongozi kwa kuwatusi wengine.
Vilevile Bw. Odinga amekejeli vita vinavyoelekezwa kwa chama cha Jubilee, akisema kwamba serikali inatishiwa na uwepo wa chama cha jubilee kuelekea siku za usoni.
Mr. Ruto must address Mr Gachagua's remarks regarding citizen shareholding and clarify his stance.
If he agrees with his deputy, then the non-shareholding majority of Kenyans will be compelled to pursue self-determination, as permitted by Kenyan and International laws. pic.twitter.com/NRvZRVHqne
— Raila Odinga (@RailaOdinga) May 22, 2023