SABINA-CHEGE

Spika wa bunge la Kitaifa Moses Wetangula, amemruhusu mbunge mteule Sabina Chege kuendelea kutekeleza wajibu wake bungeni kama naibu wa mnadhimu wa walio wachache katika bunge hilo.

Katika uamuzi wake, Spika Wetangula alieleza kwamba Muungano wa Azimio haukufuata kanuni zinazofaa kwa kuwasilisha pendekezo lao la kumbandua Sabina kutoka kwa wadhifa wake.

Hatua hiyo hata hivyo haikupokelewa vyema na viongozi wa mrengo huo ambao waliondoka bungeni mara baada ya uamuzi huo. Spika aidha ametoa mwongozo kwa muungano huo, akiwataka kujipanga na kuweka mpango unaofaa kabla ya kuwasilisha hoja hii bungeni katika kipindi cha siku 30 zijazo.

May 4, 2023