BY ISAYA BURUGU 29TH MARCH,2023-Mbunge wa Banissa, Kulow Hassan Maalim amefariki dunia baada ya kugongwa na bodaboda siku ya Jumapili katika mtaa wa South B jijini Nairobi.

Kulingana na ripoti kutoka kwa familia yake, Mbunge huyo kutoka kaunti ya Garissa alifariki mapema alfajiri ya Jumatano katika kituo kimoja cha afya alikokuwa akipata matibabu.Mbunge huyo aligongwa na pikipiki na kupata majeraha ya kichwa.

Mbunge huyo atazikwa mwendo wa saa kumi jioni ya leo Jumatano katika makaburi ya waislamu eneo la Lang’ata jijini Nairobi.Marehemu mbunge amewakilisha eneo bunge la Banissa katika Bunge la Agosti tangu 2017. Pia aliwahi kuwa mwanachama wa Kamati ya Idara ya Uchukuzi, Kazi za Umma na Makazi.

Wenzake, wakiongozwa na mbunge wa Eldas Adan Keynan wamemwomboleza kama kiongozi mashuhuri na mtumishi wa umma aliyejitolea.

March 29, 2023