BY ISAYA BURUGU,26TH APRIL,2023-Aliyekuwa mbunge wa Yatta katika kaunti ya Machakos Gedion Munyao Mutiso, ameaga dunia.Mutiso alifariki katika hospitali moja jijini Nairobi alipokuwa akipokea matibabu kutokana na ugonjwa wa saratani.Kwa mjibu wa familia yake, marehemu ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 91.

Mutiso alikuwa naibu wa marehemu  Tom Mboya kama naibu katibu mkuu wa mungano wawafanyikazi nchini.

Mwanasiasa huyo mkongwe  alihudumu awali kama afisa wa kijeshi wa kiwango cha Koplo ambapo aliondoka kwa misingi ya huruma akilalama kuhusu kile alichodai ni unyanyasaji wa wafrika chini ya utawala wa mpeperu.Mutiso aliyezaliwa tarehe 31 mwezi Machi mwaka 1932 alishiriki siasa tangu mwaka  1955.

Anafahamika kwa kusimama imara dhidi ya ulaji kiapo mwaka 1969  na kuiwakilisha Kenya katika mungano wa kibiashara wa umoja wa Afrika.Mungano huo ulikuwa muhimu kwa kuviunganisha vyama vya  KANU  na KADU vilivyoipelekea Kenya kujinyakulia uhuru wake. Amemuacha mjane Bi Pauline Mutiso,Watoto ,wajukuu na vitukuu.

 

April 26, 2023