BY ISAYA BURUGU,1ST MAY,2023-Maafisa wa polisi mjini Narok wanaendesha uchunguzi kufuatia kifo cha kutatanisha cha mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chou kikuu cha Masai mara

.Mwanafunzi huyo aliyetambuliwa kama  Adah Nyambura mwenye umri wa miaka 20 anaripotiwa kutoweka  saa tatu na robo  kabla ya mwili wake kupatikana eneo la Macedonia  viungani mwa mji wa Narok  ukiwa nusu uchi hiyo jana.

Kwa mjibu wa taarifa ya polisi ni kwamba Mpenziwe marehemu kwa jina Brian Mutai  aliripoti kutoweka kwake jana  alfajiri wakati wakiwa katika eneo la burudani la elevate lounge kabla ya mwili wake kupatika.Inahofiwa kuwa huenda marehemu alibakwa kabla ya kuuawa

.Mwili wa mwanafunzi huyo umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa ya Narok ukisubiri upasuaji.

 

 

 

 

 

May 1, 2023