BY ISAYA BURUGU 13TH APRIL,2023-Mkurugenzi mkuu wa kiwanda cha pombe cha Keroche Breweries  Tabitha Karanja amekanusha mashtaka mapya ya kukwepa kulipa ushuruMashtaka hayo  yalitokana na ombi kutoka kwa kiongozi wa mashtaka  kutaka marekebisho kwa orodha ya awali ya mashtaka ya kukwepa kulipa ushuru wa shilingi bilioni 14.5.

Mawakili wa kiwanda cha Keroche wameiambia mahakama kwenye kikao cha leo kuwa  wengetaka swala hilo kutatuliwa nje ya mahakama.

Hata hivyo , Irene Muthee, ambaye ni afisa wa mamlaka ya utozaji ushuru nchini KRA  ameiambia mahakama kuwa hapajakuwa na makubaliano  yoyote kuhusu swala hilo kusuluhishwa nje ya mahakama  kwani Keroche ingetakiwa kumjulisha kamishana wa KRA KUPITIA barua  chini ya sheria za ushuru.

Kufuatia hayo,mahakama imeipa Keroche breweries siku 45 kuanza mchakato wa kutatua swala hilo nje ya mahakama na iwapo itashindwa kufanya hivyo basi kesi hiyo itaendelea hadi kutamatika.

KRA iliishataki Keroche kwa kos ala kuidharua mahakama mwishomwisho mwa mwaka jana.

 

 

 

April 13, 2023