Baadhi ya wanaume waliochukuliwa kama mashujaa walikua na nafasi rahisi kwani wazazi wengine waliwaleta wana wao ili waolewe na shujaa huyu. Wazazi wengine pia walijishughulisha kwa kiwango kikubwa katika kuwatafutia wana wao wake.
Morans hurejelea vijana ambao wamepitia desturi ya kutoka ujana hadi utu uzima. Hii ni hatua muhimu katika utamaduni wa Wamasai.
Katika jamii ya kimaasai, hafla yoyote iliyoashiria mwanzo mpya, iliandamana na shughuli za kunyoa nywele na kubadili mavazi, ishara kamili kwamba mmoja amekubali kuyaacha yale ya zamani na kukumbatia Maisha mapya.
Baadhi ya mambo mengine ambayo vijana hawa walipaswa kutekeleza, yalitokana na mafunzo waliyopokea au kwa kutazama yale wazee na wanaume wengine katika jamii hii walikua wakitenda.
Jukumu la malezi ya Watoto katika tamaduni na jamii ya kimaasai, lilikua jukumu la wanajamii wote, kuanzia kwa wazazi wa mtoto, jamaa wa karibu, Watoto wenzake na hata jamii nzima kwa ujumla.
Katika siku ya kupewa jina kwa mtoto, familia ya mtoto ilitafuta msimamizi wa mwana wao, aliyekuwa wa jinsia moja na mtoto mwenyewe aliyefaa kutoka katika familia au ukoo tofauti na mtoto mwenyewe. Msimamizi huyu alifaa kuwa mtu mwenye maadili mema na aliyekuwa…
Ili kuwa na kizazi cha siku za usoni, Watoto huwa kiungo muhimu katika kila jamii. Katika jamii ya kimaasai, Watoto walianza kulindwa wakiwa katika tumbo la mama, na hivyo kina mama wajawazito waliangaziwa kwa njia tofauti wakilinganishwa na wanajamii wengine. Baada ya…
Uwezo wa wanawake katika jamii hii, ulidunishwa sana, kwani jamii ya wamaasai iliwainua wanaume zaidi na hivyo kuwaona wanawake kama wasio na uwezo wa kuwa viongozi