BY ISAYA BURUGU,13TH MARCH,2023-Taharuki ingali imetanda katika Kijiji cha Ngarua  kaunti ya Laikipia baada ya Watu wenye silaha kumia  kijiji hicho mapema jana  Jumapili.

Kisa hicho kilipelekea  kifo cha  mwanamume mmoja huku  ng’ombe wake wanane na kondoo 120 wakibwa.Polisi walisema kuwa marehemu alipigwa risasi tumboni kabla ya kufariki katika hospitali ya kaunti ndogo ya Ndindika.

Shambulizi hilo lilitokea mwendo wa saa tatu asubuhi katika kijiji cha Kieni ambapo watu wasiojulikana idadi yao walivamia na kufyatua risasi kuelekea marehemu alipojaribu kuingilia kati kabla ya kuondoka na mifugo hao.Mwili ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Sipili ukisubiri uchunguzi wa maiti.

Kisa hicho kilijiri kabla ya makataa ya hivi leo Jumatatu kwa wanakijiji kuondoka kwenye mapango na korongo katika eneo hilo na kaunti zingine huku serikali ikipanga awamu ya pili ya operesheni yake.Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki jana alitangaza katika miezi saba iliyopita zaidi ya Wakenya 135, wakiwemo maafisa 20, wameuawa na majambazi.

Aliwaambia wanaoishi katika baadhi ya maeneo yaliyolengwa Kaskazini mwa Rift kuondoka kufikia Jumatatu 8.30 asubuhi huku kukiwa na maswali kuhusu ni wapi wanakijiji hao watahamia.

 

March 13, 2023