Tovuti ya KUCCPS imefunguliwa tena kwa awamu ya pili ambapo wanafunzi waliotuma maombi ya kujiunga na vyuo mbalimbali watapata fursa ya kufanya masahihisho ya chaguo lao.
Zoezi hilo litawapa wahitimu wa shule za sekondari fursa nyingine ya kuomba kozi zinazotolewa katika vyuo vikuu na vyuo vya ufundi.
Zoezi hilo litaendelea hadi Juni 27, 2023.
KUCCPS pia imewataka watahiniwa waliopata gredi ya C+ na zaidi katika mtihani wa KCSE wa 2022 na hawakupata fursa ya masahihisho ya kwanza kuhakikisha kwamba wametuma maombi ya masomo ya digrii au TVET katika kipindi cha sasa.
The KUCCPS portal will open again tomorrow, June 16, 2023.
The 2022 KCSE candidates who have not secured a course are invited to login and apply again, starting tomorrow. This is also a chance for those who would like to apply for the first time.
Keep it here for more updates. pic.twitter.com/XtnllU9Iwh
— The Placement Service (@KUCCPS_Official) June 15, 2023