Tume ya kuwaajiri waalimu nchini TSC itawaajiri waalimu 30,000 mwezi januari mwaka ujao, ili kusaidia kupunguza uhaba wa waalimu katika shule mbalimbali humu nchini, hasa wakati huu taifa litakua linashuhudiwa wanafunzi wakijiunga na madarasa ya Gredi ya saba chini ya mtaala mpya wa CBC.
Mkurugenzi mtendaji wa TSC Bi. Nancy Macharia ameweka wazi kuwa tume hiyo ina uhaba wa waalimu wapatao 68,000 wa shule za upili nchini, akieleza kuwa hatua ya kuwaajiri waalimu zaidi itasaidia kupunguza uhaba huu. Aidha amedokeza kuwa waalimu wengine watalazimika kupokea mafunzo mapya ya mtaala wa CBC ili kuwawezesha kutoa mafunzo yanayofaa.
@TSC_KE CEO Dr Nancy Njeri Macharia distributes #KCSE2022 examination materials at the Nyali West container, Mombasa County
— TSC (@TSC_KE) December 2, 2022