Tume ya Kuwaajiri Walimu nchini TSC imeidhinisha uhamisho wa walimu 14,613 hadi kaunti zao za nyumbani, kama mojawapo ya njia za kufanikisha mpango wa kuwawezesha walimu kufanya kazi katika maeneo yao ya nyumbani.
Kati ya walimu elfu 14,733 waliowasilisha maombi ya uhamisho wakati dirisha la uhamisho lilifunguliwa, ni walimu 120 pekee ambao maombi yao ya uhamisho hayakuidhinishwa baada ya TSC kusema kuwa bado haijapata nafasi zao.
Walimu wakuu waliopata uhamisho wameratibiwa kuwasili katika maeneo yao ya kazi tarehe 16 mwezi huu, huku walimu wengine wakiagizwa kuwasili katika maeneo yao mapya ya kazi tarehe 23 mwezi huu, shule zitakapofunguliwa kwa muhula wa kwanza.