Tume ya kuwaajiri Walimu TSC inatazamiwa kuajiri walimu zaidi ya laki moja katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia amesema serikali itaajiri walimu ili kupunguza uhaba wa walimu wa kitaifa katika taasisi zote za kimsingi.
Macharia alizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa Tume hiyo wa 2023-2027. Bi. Macharia alidokeza kuwa Sh.134 bilioni zinatakiwa kuajiri walimu hao katika kipindi hicho cha miaka mitano.
Mnamo Juni 28, Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alitangaza kuwa serikali itaajiri walimu 25,000 kuanzia mwezi huu huku akishikilia kwamba serikali ya Kenya Kwanza imejitolea kikamilifu kuhakikisha sekta ya elimu inaimarika.
Ezekiel Machogu, @EduMinKenya Cabinet Secretary at the launch of TSC Strategic Plan 2023-2027. pic.twitter.com/Brl2DDusXz
— TSC (@TSC_KE) July 6, 2023
1/4 Ezekiel Machogu, Cabinet Secretary: @EduMinKenya: This strategic plan gives us a sense of direction that creates standards and accountability. The Plan has come at an opportune time because……
— TSC (@TSC_KE) July 6, 2023
The TSC has today unveiled new ▶️Vision and ▶️Mission statements at the Launch of the Strategic Plan 2023-2027. The new Plan takes a keen interest in teachers, as they ultimately shape learners’ lives. ▶️▶️▶️@EduMinKenya @OfficePCS_KE pic.twitter.com/S1ZTubKffr
— TSC (@TSC_KE) July 6, 2023