BY ISAYA BURUGU,18TH JULY,2023-Tume ya huduma za mahakama imemteua Athman Abdulhalim Hussein kama chifu kadhi mkuu nchini.Hussein ambaye ni kadhi zamani wa eneo la Nairobi atakuwa anachukua mahalama pa Ahmed Muhdha.
Uteuzi wake ulijiri baada ya tume hiyo kuendesha mahojiano ya wagombea waliorodheshwa kwa wadhifa huo na ambao walikuwa wametuma maombi ya nafasi hiyo iliyotangazwa tarehe 14 mwezi April mwaka huu kabla ya jaji mkuu Martha Koome jumatatu kutangaza kuwa JSC ilikuwa imemteua Hussein.
Wagombea waliokuwa wameorodheshwa na JSC ni Pamoja na Sukyan Hassan Omar, Idris Nyamagosa Nyaboga, Athman Abdulhalim Hussein, Kutwaa Mohamed Abdalla na Omari Hassan Kinyua walioshiriki kwenye mahojiano yaliyoendeshwa tarehe 22 mwezi Mei mwaka huu.
Mahakama za kadhi zilibuniwa chini ya kifungo 170 cha katiba ya Kenya na zina jukumu la kushughulikia kesi za ndoa za kislamu na Maisha ya familia kwa mjibu wa sharia na pia kushugulikia maswala ya uridhi miongoni mwa waislamu.