Tume ya kuratibu Mishahara na Marupurupu ya wafanyakazi wa umma SRC imetetea hatua yake ya kupendekeza nyongeza ya mishahara kwa maafisa wa Serikali na umma kuanzia Julai 1 huku Wakenya wengine wakikabiliana na gharama ya juu ya maisha.

Wakati wa mkutano na wanahabari siku ya Jumamosi, mwenyekiti wa SRC Lyn Mengich alisema tume hiyo ilikuwa ikitekeleza tu awamu ya tatu ya nyongeza ya mishahara iliyokubaliwa kwa watumishi wa umma.

Aliendelea kusema kwamba kwa muda wa miaka tatu maafisa wa serikali hawajapata nyongeza ya mishahara kufuatia janga la Covid-19.

Kando na hayo Mengich alifichua kuwa  wizara ya hazina ya kitaifa imetenga Ksh22.6 bilioni kwa nyongeza ya mishahara, huku 40% ikienda kwa walimu (Ksh9.1 bilioni), 30% kwa utumishi wa umma (Ksh6.7 bilioni), 27% kwa serikali za kitaifa na kaunti na 3. % kwenda kwa maafisa wa serikali (Ksh574 milioni).

July 1, 2023