Rais William Ruto amesema kuwa hatakubali kutishwa kwa semi za maandamano zinazoenezwa na viongozi wa upinzani, akisema kwamba Taifa la Kenya linaongozwa na katiba na wala hakuna mkenya aliye na kibali cha kuwatisha wakenya wengine.

Akizungumza katika ikulu ya Nairobi alipokutana na viongozi wa kaunti ya Transzoia, Ruto alitoa Onyo kwa upinzani dhidi ya kusambaratisha au kuhitilafiana na biashara za wananci wengine wanao jitafutia riziki ya kila siku.

Usemi wa rais umeungwa mkono na naibu wake Rigathi Gachagua Pamoja na mkuu wa mawaziri serikalini Musalia Mudavadi, ambao wamesema kuwa wakati umefika kwa Bw. Odinga kufuata mkondo unaofaa, huku wakikosoa tangazo la siku ya mapumziko mnamo tarehe 20 mwezi huu.

 

March 15, 2023