Waziri wa ulinzi nchini Aden Duale amesema taifa la kenya litaendelea kupambana ima fa Ima na wanamgambo wa kundi la Al Shabaab.
Akizungumza leo wakati wa sherehe ya kuhitimu kwa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Garissa, Waziri Duale amesisitiza kuwa serikali itatumia nguvu zote zilizopo kuondoa kitisho cha ugaidi nchini na kuwahakikishia Wakenya usalama.
Aidha amepongeza hatua zilizopigwa kwenye chuo hicho, ambacho kilivamiwa na wanamgambo wa kundi la Alshabaab mwaka wa 2015 waliosababisha vifo vya wanafunzi 147. Duale pia amemwomba waziri wa Elimu Ezekiel Machogu kukitengea chuo hicho nafasi za wanafunzi wapatao 3000 ili kukisaidia kuimarika hata zaidi.