KINDIKI KITHURE - Radio Osotua

 BY ISAYA BURUGU 11TH JULY, 2023-Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ametoa hakikisho kuwa hatimaye kila mtu aliyechangia kufanikisha mauji hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

Waziri  amesema hayo alipofika mbele ya kamati ya seneti inayochunguza mauji ya Shakahola iliyotaka kufahamu ni kwa nini uchunguzi huo unaonekana kujikokota.Waziri amesema tatizo la shakahola linapaswa kushughulikiwa na kila mhusika nchini kwani linawahsisha watu wengi.

Pia amesema sheria pia inachangia katika mwendo wa polepole wa kushughulikia swala hilo kwani swala hilo ni nyeti mno na ni sharti uchunguzi wa kina kuendeshwa kwa kuzingatia sheria na kila ushahidi kubainishwa kikamilifu kabla ya sheria kuchukua mkondo wake.

.Waziri pia amelezea umuhimu ulioko kuwapa msaada wakisaikologia vijana wanaotumiwa kufukua makaburi waliomozikwa watu waliofariki kwani wanausumbufu wakimawazo.

Haya yanajiri siku moja baada ya awamu ya nne ya ufukuaji wa maiti kuendelea katika eneo hilo ambapo milli kumi na mbili Zaidi ikifukuliwa huku ikiaminika kuwa watu  Zaidi walizikwa kwenye  makaburi 40  yanayotarajiwa kufukuliwa.

 

 

 

 

July 11, 2023