BY ISAYA BURUGU 27TH JUNE 2023-Maafisa wa Polisi wameanzisha msako dhidi ya kundi la  vijana linaloripotiwa kuvamia duka mmoja eneo la wasonyiro Narok kusini kwa madai ya mwenye duka hilo kudaiwa kujihusisha na ulawiti na ndoa za jinzia  moja.

kamanda wa polisi Narok ya kati John Momanyi ameellani tukio hilo akisema ni hatia kwa wananchi kuchukua sheria mikononi mwao bila kupiga ripoti kwa mafisa wa polisi .

Kamanda huyo wa polisi amesema yeyote atakapatika atashtakiwa kwa mujibu wa sheria.

Momanyi amedokeza kuwa bado hakuna mtu ambaye ametiwa mbaroni kufikia sasa baada ya duka la mfabiashara  huyo kuchomwa moto.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

June 27, 2023