Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome amesema uchunguzi unaendelea ili kuwafikisha mahakamani watu waliovamia kiwanda cha gesi cha East Africa Specter kinachomilikiwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga na kipande cha ardhi kinachomilikiwa na familia ya aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta.
Wahalifu hao walivamia ardhi ya familia ya Kenyatta kando ya barabara ya Nairobi Eastern Bypass siku ya Jumatatu asubuhi, na kukata miti sawa na kuwaiba kondoo, saa chache baada ya kampuni ya gesi ya Odinga kushambuliwa na madirisha kadhaa kuvunjwa.
Kupitia taarifa IG Koome ameeleza polisi walipokea ripoti za uvamizi katika kiwanda cha Embakasi na walijibu haraka na kuzuia uhalifu zaidi.
PRESS STATEMENT
CONDEMNING VIOLENCE AGAINST POLICE DURING AZIMIO LA UMOJA-ONE KENYA ALLIANCE DEMONSTRATIONS pic.twitter.com/hcejWQ15NZ
— National Police Service-Kenya (@NPSOfficial_KE) March 28, 2023