Chama tawala cha UDA ambacho ni mojawapo ya vyama tanzu katika muungano wa Kenya kwanza, kimebadilisha usimamizi wake, na kuwapata viongozi wapya waliokabidhiwa jukumu la usukuma gurudumu la uongozi.

Katika mabadiliko hayo, Gavana wa kaunti ya Embu Cecily Mbarire ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa chama na kutwa amahala pake seneta wa zamani wa Machakos Johnson Muthama aliyejiuzulu ili kupata fursa ya kuhudumu kama mjumbe wa Tume ya Bunge.

Mwingine aliyepata nafasi chamani humo ni seneta wa zamani wa Kakamega Cleophas Malala ambaye ametwaa wadhifa wa katibu mpya wa chama na anachukua nafasi ya Seneta mteule Veronica Maina.

Kwa upande wake, Katibu mpya wa chama hicho ameeleza imani yake ya kuinua na kukuza chama cha UDA katika kipindi cha uongozi wake. Wote walioteuliwa watahudumu kikaimu hadi pale wanachama wa kitaifa watakapoandaa uchaguzi wa viongozi wa kuongoza chama kwa muda mrefu.

 

February 27, 2023