Viongozi wa chama cha UDA wametangaza mipango ya kupinga maandamano ambayo yameratibiwa kufanyika siku ya jumatatu na kiongozi wa azimio la umoja Raila Odinga.

Mojawapo wa mipango hiyo ni kuandamana hadi katika makaazi ya bw. Odinga atakapokuwa akiwaongoza wafuasi wake kuelekea katika ikulu ya rais.

Katibu mkuu wa UDA Cleophas Malala amesema kuwa atawaongoza wafuasi wa UDA hadi Karen na kumonya bw. Odinga dhidi ya maandamano ya fujo.

March 18, 2023