Uongozi wa polisi nchini umelaani ghasia zisizo na msingi dhidi ya maafisa waliotumwa kudumisha sheria na utulivu wakati wa maandamano ya Jumatatu.
Katika taarifa, Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome, huku akiwapongeza maafisa hao kwa kujitolea kwao katika kuhakikisha amani inakuwepo, amesema maafisa 7 walijeruhiwa huko Nyanza huku watu 25 wakikamatwa wakati wa maandamano hayo.
Katika mji mkuu wa Nairobi, jumla ya watu 213 walikamatwa na magari 10 ya polisi yakiwa yameharibiwa.
Aidha IG aliwashutumu viongozi wa Muungano wa Azimio One Kenya na wafuasi wao kwa kufanya maandamano haramu katika miji ya Nairobi na Kisumu wakidai kupinga gharama ya juu ya maisha ila kwa maana halisi, lengo lao pekee lilikuwa kuivamia Ikulu.
PRESS STATEMENT ON VIOLENCE AGAINST NATIONAL POLICE SERVICE OFFICERS BY SUPPORTERS OF AZIMIO-ONE KENYA ALLIANCE DEMONSTRATORS. pic.twitter.com/DBwnV6uxiD
— National Police Service-Kenya (@NPSOfficial_KE) March 21, 2023