BY  ISAYA BURUGU,05,2023-Mhubiri tata Paul Mackenzie na watu wengine saba wameregeshwa mahakamani huko Shanzu hivi leo huku kesi ya mauaji inayowakumba ikiendelea.Upande wa mashtaka unaitaka mahakama kuagiza Mackenzie na watuhumiwa wengine kuzuiliwa kwa siku 90 zaidi ili kuwaruhusu polisi kukamilisha uchunguzi.

Vilevile upande wa mashataka umepinga kuachiliwa kwake huru ukisema kuwa Hapana hakikisho kuwa hawatakwenda kumalizia mauaji waliyoanzisha katika msitu wa shakahola kule Chakama kaunti ya Kilifi. Katika kikao cha mahakama cha asubuhi hii ,upande wa mashataka umedai kuwa ikizingatiwa Mackenzie ametekeleza makosa mbali mbali siku zilizopita yaliyoishia kutiwa mbaroni kwake,haitaji tena kupewa dhamana

.Ikizingatiwa makosa wanayotuhumiwa ,upande wa mashataka unadai kuwa kuendelea kuzuiliwa kwao,ni kwa manufaa kwani wakiwa kizuizini usalama wao pia umehakikishiwa.

 

 

 

 

May 5, 2023