Chama cha Muungano wa Azimio la Umoja kimetangaza kikosi cha Viongozi saba wanaotarajiwa kuwakilisha mrengo huo katika mazungumzo ya kutafuta mwafaka katika shughuli ya uteuzi wa makamamishena wa tume ya IEBC.
Chama hicho kinachoongozwa na Raila Odinga kimetaja orodha hiyo, kama mojawapo ya matakwa waliyopendekeza kuelekea kwa mazungumzo hayo yaliyotangazwa na Rais William Ruto. Viongozi waliotajwa katika orodha hiyo ni:
- Seneta wa Narok Ledama Ole Kina
- Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna
- Seneta wa Kitui Enoch wambua
- Mbunge wa Malindi Amina Mnyanzi
- Mbunge wa Mbita Millie odhiambo
- Mbunge wa Pokot Kusini David Kosing
- Mbunge wa Rarieda Otiende Amolo
Muungano huo ulipendekeza kamati maalum itakayoendesha mazungumzo hayo nje ya bunge, jambo ambalo limepingwa vikali na muungano wa Kenya kwanza.
Kinara wa Muungano huo aidha alitangaza kwamba mpango wa kuandaa maandamano ungali hai iwapo mikakati ya mazungumzo haya haitazaa matunda yoyote.
John F. Kennedy once stated, 'Civility is not a sign of weakness, and sincerity is always subject to proof.'
We accepted the call for dialogue but shall defend all our constitutional rights.
We won't hesitate to call for demonstrations if the process doesn't yield results. pic.twitter.com/UOySf4iFka
— Raila Odinga (@RailaOdinga) April 6, 2023
The following Hon. Members have been nominated to rep Azimio in the dialogue;
1) Hon. Ledama Ole Kina
2) Hon. Edwin Sifuna
3) Hon. Enock Wambua
4)Hon. Amina Mnyazi
5) Hon. Millie Mabona
7) Hon. Otiende Amolo— The ODM Party (@TheODMparty) April 6, 2023