BY ISAYA BURUGU ,OCT 13,2022-Mahakama kuu imetupilia mbali, kesi ya kuharibia jina iliyokuwa iiliyowasilishwa mahakamani na kampnuni ya maziwa ya Brookside Dairy limited dhidi ya mbunge wa Nyali Mohamed Ali.
Jaji Hedwig Ongudi amesema kuwa kesi hiyo iliyokuwa imewasilishwa mbele ya kitengo cha katiba inapaswa kuwasilishwa kwenye kitengo kinachostahili cha mahakama.
Katika kesi hiyo Brookside ilikuwa imemshtaki Mohamed Ali kwa kudaiwa kuwachochea wananchi ili kuadhiri kiuchumi na kibiashara shughuli za kampuni hiyo.
upande wake Ali aliwasilisha pingamizi akisema kuwa kuna haki zake msingi ambazo zimekiukwa na akaitaka mahakama kufutilia mbali kesi hiyo.
Mbunge huyo kupitia wakili wake Adrian Kamotho alikuwa amedai kuwa nguzu za mahakama zilikuwa zimetumiwa visivyo kwani hatua ya kuendeleza kesi hiyo ni kinyume cha matarajio ikizingatiwa kuwa brookside ni kampuni ya kibinafsi.Kesi hiyo imetupiliwa mbali.