Bunge la kitaifa hivi leo limeidhinisha uteuzi wa Dkt. David Oginde kama mwenyekiti mpya wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC.

Dkt. Oginde aliteuliwa na rais kutwaa wadhifa huo kufuatia kukamilika kwa kipindi cha kuhudumu cha Askofu Mstaafu wa kanisa la kiangalikana Eliud Wabukala. Naibu mwenyekiti katika kamati ya Haki na Masuala ya Kisheria katika bunge hilo (JLAC) Mwengi Mutuse, aliunga mkono na kusisitiza kwamba uteuzi wa Dkt. Oginde katika wadhifa huo utawezesha taifa kupambana vyema na jinamizi la ufisadi.

 

April 20, 2023