Vatican imetangaza mazishi ya Papa yatafanyika Jumamosi, Aprili 26 kuanzia saa 10:00 asubuhi.Papa Francis atapelekwa kwenye Basilica ya St Peter siku ya Jumatano asubuhi saa 09:00.

Jeneza la Papa liatasalia katika basilibca ya St. Peter’s hadi  siku ya mazishi ilikuwapa waumini fursa kutoa heshima zao za mwisho.Mwili wake kwa sasa umewekwa kwenye jeneza katika kanisa la makazi ya Santa Marta, ambapo aliishi wakati wa upapa wake wa miaka 12.

Vatican ilikuwa imetangaza hapo awali kwamba Papa Francis alifariki kutokana na kiharusi.Papa alifariki Jumatatu ya Pasaka, Aprili 21, 2025.

Mkurugenzi wa idara ya Afya na Usafi wa Jimbo la Vatican, Andrea Arcangeli alitoa cheti rasmi cha kiini cha kifo cha Papa. Mazishi ya Papa Francis yatafanyika nje, mbele ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro.

Mkuu wa Chuo cha Makardinali, Giovanni Battista Re, ataongoza ibada hiyo.

April 22, 2025

Leave a Comment