Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro, akizungumza na wanahabari, katika hafla ya kupeana hundi za masomo kwenye uwanja wa Mumbi, Murang’a, Ijumaa 09. Juni 2023.


Mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa na ambaye pia ni mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro, amesema kwamba mswada wa fedha bado uko wazi kwa marekebisho zaidi ili kuhakikisha kwamba sauti ya wananchi inapata nafasi kwenye mswada huo.

Mbunge huyo amesema kwamba kamati ya fedha imekuwa ikizunguka maeneo tofauti ya taifa ili kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo yaliyo kwenye mswada huo.

Akizungumza katika uwanja wa Mumbi, Murang’a alipokuwa akitoa hundi za masomo ya bursary kwa wakazi, Nyoro alieleza kuwa kutakuwa na nafasi ya mazungumzo zaidi kabla ya mswada huo kupitishwa, huku akieleza kwamba Rais William Ruto pia anashauriana na viongozi wengine kuhusu mswada huo.

June 9, 2023