Rais William Ruto amewateua watu 50 katika nyadhifa za mawaziri waratibu (almaarufu CAS) katika wizara mbalimbali nchini, wanaotarajiwa kupigwa msasa na Bunge kabla ya kuidhinishwa kwa uteuzi wao.

Miongoni mwa walioorodheshwa katika orodha hiyo ya Makatibu waratibu ni Pamoja na aliyekuwa gavana wa Narok Samuel Tunai na aliyekuwa mbunge Mteule Millicent Omanga walioteuliwa kuhudumu katika wizara ya usalama wa ndani, aliyekuwa mbunge wa Mumias Mashariki Benjamin Washiali na mwenzake mbunge wa zamani wa Rarieda Nicholas Gumbo ambao wameteuliwa katika wizara ya Uchukuzi.

Wengine waliovuna katika uteuzi huu ni Pamoja na :

Dennis Itumbi – wizara ya teknolojia na mawasiliano, Bishop Margaret Wanjiru – wizara ya mashirika na Biashara ndogo na za Kadri.

Wesley Korir na Charles Njagua – Wizra ya michezo na masuala ya Vijana

Wilson Sossion – Wizara ya utalii.

March 16, 2023