Utekaji Nyara

Vijana wanne kati ya sita waliokuwa wametekwa nyara mwezi uliopita wameachiliwa huru na kuungana na familia zao mapema leo. Kulingana na jamaa wa Billy Mwangi, Peter Muteti, Bernard Kavuli na Rony Kiplangat, walipokea mawasiliano kutoka kwa vijana hao huku Mwangi na Muteti wakiripotiwa tayari kukutana na familia zao.

Wanne hao walikuwa miongoni mwa kundi la vijana sita waliotekwa nyara, huku serikali ikiendelea kujitenga na madai ya kuhusika katika visa vya utekaji nyara. Hata hivyo, hadi kufikia wakati wa kuandaa taarifa hii, bado haijabainika walipo Gideon Kibet, anayejulikana kwa jina maarufu la Kibet Bull, pamoja na Steve Mbisi.

Habari za kuachiliwa kwa vijana hao wanne zimeibuka katika siku ambapo vijana kwenye mitandao ya kijamii wanapanga kushiriki maandamano ya kushinikiza haki na kukomeshwa kwa visa vya utekaji nyara nchini.

January 6, 2025

Leave a Comment