Fedha

Jopo la majaji watatu walioteuliwa kusikiliza na kuamua kesi inayohusu uhalali wa sheria za fedha za mwaka 2023 limeanza vikao vyake leo kwenye mahakama ya Milimani. Majaji hao, Jaji David Majanja, Jaji Christine Meoli, na Jaji Lawrence Mugambi, wanatarajiwa kufanya maandalizi muhimu kwa ajili ya kuanza kusikiliza kesi hiyo.

Kesi hii iliwasilishwa mahakamani na walalamishi saba wanaopinga vipengee kadhaa vilivyomo kwenye sheria hizo za fedha za mwaka 2023, pamoja na utekelezaji wake. Majaji hao na wahusika wengine kwenye kesi hii wametumia vikao vya leo kuweka utaratibu wa kusikiliza kesi hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoa muda wa kutosha kwa pande zote kutoa hoja zao. Awali, Mahakama Kuu ilikuwa imeamuru kusitishwa kwa utekelezaji wa sheria hizo, lakini agizo hilo lilikataliwa na Mahakama ya Rufaa.

Katika vikao vya leo, ombi la seneta wa Kaunti ya Busia na mwanaharakati Okiya Omtatah la kuwauliza maswali mahakamani maspika wa mabunge ya kitaifa limekataliwa. Omtatah amedai kuwa Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetangula, na mwenzake wa Seneti, Amason Kingi, wametoa taarifa za uongo kwenye hati-kiapo zilizowasilishwa mahakamani.

https://twitter.com/Kenyajudiciary/status/1688414487810838528?s=20

August 7, 2023