BY ISAYA BURUGU,20TH APRIL,2023-Mungano wa Azimio la umoja umeandaa mkutano wake  wa kukutana na wananchi mjini Muranga kaunti ya Muranga hivi leo.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wanaoegemea murengo huo,wakiwemo Raila Odinga,Martha Karua,Jeremiah Kioni,Kalonzo Muysoka na Wycliff Oparanya, Eugine Wamalwa kati ya Wengine.Mkutano huo umeandaliwa licha ya polisi kuwema kuwa si halali.Wakaazi waliohudhuria mkutano huo wametoka katika kaunti zote ndogo saba za kaunti ya Muranga.

Lengo la mkutano huo kwa mjibu wa aliyekuwa gavana wa Muranga Mwangi wa Iria unanuia kuangazia  maswala  yanayowakumba wakazi wa Muranga.

Waliozungumza kwenye kikao hicho wameguzia changamoto mbali mbali zinazowakumba wanachi wakiwemo wakulima wa kahawa na majani chai kaunti ya Muranga.

 

 

 

 

 

April 20, 2023