Viongozi wa Muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamepokea kwa furaha taifa la Somalia kama mwanachama wa nane. Hatua hii rasmi ilitangazwa rasmi wakati wa Kikao cha 23 cha Marais kilichofanyika mjini Arusha, Tanzania, ambapo marais na wakuu wa mataifa wanachama walijumuika.
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, alipokelewa kwa mikono miwili miezi kadhaa baada ya pendekezo la kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitishwa na marais na wakuu wa mataifa wanachama. Hii inaashiria hatua muhimu kwa Somalia katika kuimarisha uhusiano wake na mataifa mengine ya Afrika Mashariki na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi na kisiasa kwenye eneo hilo.
Katika kikao hicho, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Uteuzi huo unathibitisha jukumu la Sudan Kusini kama taifa lenye uongozi katika kukuza ushirikiano na maendeleo ya kanda.
🔺23rd Ordinary Summit of the EAC Heads of State.
📌 The EAC Summit of Heads of State admits the Federal Republic of Somalia as the 8th Member of the EAC in accordance with Article 3 of the Treaty for the Establishment of the EAC@TheVillaSomalia @HassanSMohamud @pmathuki pic.twitter.com/bqmPLtIsCn
— East African Community (@jumuiya) November 24, 2023
SOMA PIA:Serikali yaahirisha mpango wa kufungua tena vituo vya mpaka kati ya Kenya na Somalia.