BY ISAYA BURUGU 28TH JUNE,2023-Viongozi wa dini ya kislam wametoa wito wa kudumishwa kwa amani humu nchini na kujiepusha na mambo yanayoweza kuyumbisha umoja wa kitaifa.
Wakizungumza kule Mombasa,wakati wa kuanza kwa sherehe za Idd-Adha,pia wametoa wito kwa watu wote wenye uwezo kushiriki walicho nacho na wasiokuwa na uwezo katika jamii ikiwa ni njia moja ya kutoa shukrani zao kwa mungu.
Viongozi hao pia wamewaomba viongozi wa kisiasa wakiwemo wale wa serikali kujitahidi katika kubuni mazingira yenye amani na utulivu nchini kwa minajili ya ustawi wakitaifa.Kuhusu utata ulioko baina ya serikali na upizani,
viongozi hao wanasema ni sharti pande hizo mbili kuketi chini kwenye meza ya mazungumzo na kusaka suluhu kwa tofauti baina yao.Wameongeza kuwa kuna njia mbadala za kusuluhisha utata ulioko na kutaka upinzani kisitisha wito wa mandamano.
.