BY ISAYA BURUGU 11TH JULY,2023-Baadhi ya viongozi wa kidini katika kaunti ya Kisumu wameitaka serikali kuitisha mazungumzo yatayoleta amani nchini ili kuzuia mkwamo wa kisiasa na mzozo unaoshuhudiwa nchini.Viongozi hao wakizungumza na wandishi Habari hivi leo wamesema serikali inapaswa kuchukulia kw auzito wananchi wanaoandamana na kuonyesha moyo wa kujali changamoto zinazopelekea mandamano hayo.

Huku wakisisitiza kuwa mandamano yanayoandaliwa na mungano wa Azimio la Umoja ni halali kisheria,viongozi hao pia wanawataka wandamanaji kufanya mandamano yao kwa amani.

.Aidha wanapendekeza serikali kuheshimu uamuzi wa mahakama kuhusu sheria yakifedha ya mwaka 2023 na kusubiri mkondo wa sheria kutekeleza wajibu wake kikamilifu kuhusu sheria hiyo na wala isitekelezwe kwa sasa

.

 

 

 

July 11, 2023