BY ISAYA BURUGU,28TH MARCH,2023- Hali ya taharuki imesalia  kutanda katika mtaa wa kibra jijini Naiobi baada ya wakaazi kuamka na kukadiria hasara iliyowakuma kufuatia maandamano ya kupinga serikali yaliyofanyika hiyo jana.Makumi ya watu wameonekana  wakichukura kwenye vifusi  ili kujaribu kukoa  kilichoachwa na moto mkubwa uliozuka jana jioni.Miongoni mwa wanaokadiria hasara ni  Pamoja na wafanyibaishara kutoka eneo hilo .Mfanyibiashara mmoja aliyetambuliwa kama John  alipoteza duka la kuuza vifaa vya ujezni na sa baa.Anasema kuwa  baa hiyo ambayo ndio iliyokuwa tegemeo lake ilikuwa na bidhaa za dhamani ya karibu shilingi milioni 4   kufikia hiyo jana.kufikia leo asubuhi kilichosalia ilikuwa ni majibu ,mawe na mabati yaliyoteketea.Aidha kanisa la PCEA mtaani humo liliteketezw ana wahuni.Mhubiri Sarah Muriithi anayehudumu katika kanisa hilo amesema wahuni hao waliharibu jingo la kanisa hilo kabla ya kuliteketeza moto,Hawajawezi kukadiria hasara iliyowafika ambayo anasema ni kubwa.

Wakati huo huo viongozi wa madhehebu mbali mbali wamelaani mashambulizi na uharibifu uliyosababishwa kwa makanisa  na hata mali ya watu binafsi mtaani wa Kibra hiyo jana.Viongozi hao waliojumuisha viongozi wa dini ya kislam,wamefika katika mtaa huo na kuandaa maombi ya Pamoja kabla ya kuwahutubia wandishi Habari.Kuharibiwa kwa makanisa kukishutumiwa vikali.Pia wanaitaka serikali kuwasaka na kuwachukulia hatua waliofanya kitendo hicho.

Viongozi hao wakiwasihi viongozi wakisiasa kufanya mashauriano ili kuwe na mapatano ili kuzuia nchi kugawanyika.

 

 

 

 

 

 

 

 

March 28, 2023