Visa vya kipindupindu vilivyoripotiwa nchini sasa vinafikia 7,570, kutoka 6,391 kufikia Machi 7, data ya hivi karibuni kutoka kwa Wizara ya Afya inaonyesha.
Ripoti ya hali ya kila siku ya mlipuko wa kipindupindu inaonyesha kufikia Machi 23, vifo vya ugonjwa huo vilifikia 121.Hili ni ongezeko la 22 kutoka Machi 7 wakati vifo vilikuwa 99.
Kesi ya kwanza iliripotiwa Oktoba 5, 2022.Vifo sita viliripotiwa katika siku 10 zilizopita watu watatu kutoka Nairobi, wawili kutoka Mandera na mmoja kutoka Wajir.
Kufikia sasa kaunti 17 zimeripoti visa vya kipindupindu huku Garissa ikiwa na visa vingi zaidi 2,163 ikifuatiwa na Mandera 1,464, Nairobi 1,196, Tana River 762 na Wajir ina visa 655.
Kaunti zingine ni pamoja na Kiambu 402, Machakos 388, Kajiado 235, Meru 85, Nyeri 55, Homa Bay 51, Murang’a 44, Kitui 27, Pokot Magharibi 16, Nakuru 13 Uasin Gishu nane na Bomet sita.
Kaunti saba ambazo ugonjwa huo umedhibitiwa ni pamoja na Homa Bay, Kitui, Meru, Nyeri, Uasin Gishu na Pokot Magharibi.
Katika siku 10 zilizopita, kaunti za Mandera, Kajiado na Wajir zimekuwa na viwango vya juu zaidi vya mashambulio vya asimilia 19.4, 8.6 na 7.5 kwa kila watu 100,000 mtawalia.