Kenya imeungana na ulimwengu hivi leo kuadhimisha siku ya afya ya akili huku visa vya watu walio na matatizo ya akili vikiripotiwa kuongezeka.Humu nchini inakisiwa kati ya watu 6 watano wana tatizo la kiakili. Sababu mbali mbali zinaripotiwa kusababisha matatizo ya kiakili nyingi zikijumuisha,changamoto za kiuchumi,msongo wa mawazo,sababu za kiasili kama vile familia iliyo na changamoto za kiakili kati ya nyingine.
Siku hii huadhimishwa kote duniani ili kutoa hamasisho kuhusu umuhimu wa kuwa na afya nzuri ya kiakili.Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwneguni siku hii hutoa fursa kwa wote wanaojihusisha na afya ya kiakili kuzungumza kuhusu kazi yao.
Globally, an estimated 1 in 6 working-age adults have a mental disorder. My @LinkedIn piece offers a summary of recommendations for tackling the taboo of #mentalhealth at work – it’s smart for health, for work and for the economy. #WorldMentalHealthDayhttps://t.co/CW1cqOnsHj
— Tedros Adhanom Ghebreyesus (@DrTedros) October 9, 2022
Aidha siku hii huangazia juhudi zinazowekwa kukabili tatizo hilo na yanayosalia kufanywa katika kutafuta suluhu.Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni kufanya afya ya kiakili kuwa kipau mbele kwa wote duniani.