BY ISAYA BURUGU,11TH FEB,2023-Visa vya ndoa na mimba za mapema vinaendelea kushuhudiwa katika maeneo ya mashinani Kaunti ya  Narok kutokana na wazazi wa watoto wanaodhulumiwa kuungana na wale ambao wanatekeleza maovu hayo kwenye jamii.

Haya ni kwa mujibu wa kamishna wa Narok Isaac Masinde ambaye amesisitiza kwamba visa vingi vya watoto kudhulumiwa hukosa kurepotiwa kutokana na wanaotegemewa kurepoti visa hivyo kuamua kushirikiana na wakiukaji wa haki hizo za watoto na kukubaliana kuskizana wenyewe.

kamishna Masinde ametoa changamoto kwa wazazi kukomesha tabia hiyo na badala yake kuungana na serikali katika kuhakikisha kwamba haki za watoto zimelindwa vilivyo.

Ameshikilia kwamba ni sharti watoto hao wapewe haki yao ya kupata elimu kwani taifa linawatazamia wawe viongozi katika siku za usoni..

 

February 11, 2023